CHIMBO
1

Bei za Madini Leo

Bei elekezi kutoka Tume ya Madini Tanzania
Ona Bei Zote Ilisasishwa: 7 siku zilizopita
Dhahabu
Gold
Dunia (USD/toz) $4,367.88
Dunia (TZS/g) TZS 365,119.30
Soko la Madini TZS 328,607.37
Kituo cha Ununuzi TZS 321,304.98
Fedha
Silver
Dunia (USD/toz) $67.10
Dunia (TZS/g) TZS 5,609.02
Soko la Madini TZS 5,048.11
Kituo cha Ununuzi TZS 4,935.93
Shaba
Copper
Dunia (USD/toz) $6.59
Dunia (TZS/g) TZS 550.87
Soko la Madini TZS 495.78
Kituo cha Ununuzi TZS 484.77
Tanzanite
Tanzanite
Dunia (TZS/g) TZS 2,270.44
Soko la Madini TZS 2,043.40
Kituo cha Ununuzi TZS 1,997.99

Habari za Hivi Karibuni

Angalia Zote

TUME YA MADINI YAFUNGUA DIRISHA LA FURSA KWA WAWEKEZAJI NA WANANCHI

27 Sep 2026 • 10:56
Picha TUME YA MADINI YAFUNGUA DIRISHA LA FURSA KWA WAWEKEZAJI NA WANANCHI
GEITA

Wadau wa madini, wawekezaji na wananchi kwa ujumla wamealikwa kutembelea banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Kitaifa ya Tisa ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bomba Mbili mkoani Geita, kuanzia Septemba 23 hadi Oktoba 3, 2026.

Banda hilo limekuwa sehemu muhimu kwa wananchi wanaotaka kujifunza na kupata taarifa za moja kwa moja kuhusu fursa zinazopatikana katika Sekta ya Madini, huku likitoa nafasi kwa wachimbaji, wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi kuzungumza na wataalamu na kupata ufafanuzi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Tume ya Madini.

Katika maonesho hayo, wananchi wanapata fursa ya kujifunza kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini, shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini, uchenjuaji pamoja na biashara ya madini na taratibu mbalimbali zinazohusiana na shughuli hizo.

Moja ya vivutio vinavyowavutia wananchi katika banda hilo ni Maabara ya Tume ya Madini, inayotoa elimu kuhusu huduma za upimaji na uchambuzi wa madini kwa kutumia teknolojia mbalimbali, ikiwemo mashine ya XRF inayotumika katika upimaji wa madini ya metali.

Kwa wananchi wengi, fursa hiyo inawapa nafasi ya kuona kwa vitendo namna teknolojia inavyotumika katika kutambua na kuchambua madini, huku wachimbaji na wafanyabiashara wakipata uelewa kuhusu umuhimu wa kupima madini na kupata taarifa sahihi kabla ya kufanya maamuzi ya kibiashara na uwekezaji.

Aidha, wageni wanaotembelea banda la Tume ya Madini wanapata nafasi ya kukutana na wadau wa madini waliofanikiwa, kusikiliza uzoefu wao na kujifunza namna walivyobadilisha fursa za madini kuwa shughuli zenye tija na manufaa kiuchumi.

Ushuhuda huo unaifanya safari ya kutembelea banda hilo kuwa zaidi ya kutazama maonesho, kwani wananchi wanapata nafasi ya kujifunza, kuuliza maswali, kupata ushauri wa kitaalamu na kuona fursa mbalimbali zinazopatikana katika mnyororo mzima wa Sekta ya Madini.

Kwa mwekezaji anayetafuta fursa mpya, mchimbaji anayehitaji elimu na huduma za kitaalamu, mfanyabiashara anayetaka kufahamu taratibu za biashara ya madini au mwananchi anayetamani kuelewa zaidi kuhusu Sekta ya Madini, maonesho hayo yanatoa fursa ya kupata taarifa moja kwa moja kutoka kwa wataalamu wa Tume ya Madini.

Tume ya Madini inawahimiza wananchi na wadau mbalimbali kuchangamkia fursa hiyo kwa kutembelea banda lake katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bomba Mbili, Geita, na kujifunza zaidi kuhusu fursa, teknolojia, huduma na mafanikio katika Sekta ya Madini kabla ya kufungwa kwa maonesho hayo Oktoba 3, 2026.
69 Watazamaji
HUSSEIN MAHAMUDU

PAKUA APP SASA

26 Sep 2026 • 00:35
Video
Pakua chimbo app Sasa ukutane na FURSA na wadau mbalimbali katika sekta ya madini
88 Watazamaji
HUSSEIN MAHAMUDU

FUNGUA FURSA

26 Sep 2026 • 00:32
Picha FUNGUA FURSA
Maonesho ya 9 ya teknolojia ya madini geita
88 Watazamaji
HUSSEIN MAHAMUDU

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI: Barrick Mining Corporation Jobs in Tanzania – 5 Open Positions

21 Sep 2026 • 17:14
Picha TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI: Barrick Mining Corporation Jobs in Tanzania – 5 Open Positions
Job Description
Barrick Mining Corporation is recruiting for 5 open jobs in Tanzania, creating opportunities for professionals with experience in geology, mining operations, heavy mobile equipment, project management, technical training, and surveying. As a major mining company, Barrick Mining Corporation’s activities focus on mineral exploration, development, mining operations, and the technical functions required to operate mining assets safely and effectively.
This September 2026 recruitment round includes opportunities in Shinyanga, Tarime in the Mara Region, and positions listed at the Tanzania country level. The vacancies cover technical, operational, training, maintenance, and project leadership functions, making this recruitment particularly relevant to candidates seeking careers within Tanzania’s mining sector. Applicants should carefully review the requirements for their preferred position through the official Barrick Mining Corporation careers portal before submitting an application.

Job Listings
Geology Technician
• Employer: Barrick Mining Corporation
• Location: Shinyanga, Tanzania, United Republic of
Contract/employment type: Not specified in the provided job listing
• Posting Date: September 15, 2026

Cable Bolter Trainer
Employer: Barrick Mining Corporation
Location: Tarime, Mara Region, Tanzania, United Republic of
Contract/employment type: Not specified in the provided job listing
Posting Date: September 12, 2026

Mechanic HME
Employer: Barrick Mining Corporation
Location: Tarime, Mara Region, Tanzania, United Republic of
Contract/employment type: Not specified in the provided job listing
Posting Date: September 9, 2026


Capital Project Superintendent
• Employer: Barrick Mining Corporation
• Location: Shinyanga, Tanzania, United Republic of
Contract/employment type: Not specified in the provided job listing
• Posting Date: September 3, 2026

• Survey Technician
• Employer: Barrick Mining Corporation
• Location: Tanzania, United Republic of
Contract/employment type: Not specified in the provided job listing
• Posting Date: July 8, 2026
Application Instructions
To apply go to the Barrick Mining Corporation careers portal and select job you want to apply.
Applicants should review the full vacancy details and requirements for their chosen position on the recruitment portal before completing their application.
126 Watazamaji
HUSSEIN MAHAMUDU

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI: Accountant and Sales and Marketing Representative jobs at DOMAKA September 2026

21 Sep 2026 • 16:55
Picha TANGAZO LA NAFASI YA KAZI: Accountant and Sales and Marketing Representative jobs at DOMAKA September 2026
2 job vacancies at DOMAKA
1. Accountant
Company: DOMAKA

Location: Buguruni-Sheli, Dar es Salaam, Tanzania

Job Type: Full-Time / Permanent

About the Role
DOMAKA is looking for a qualified, highly motivated, and dedicated individual to fill the position of Accountant. In this role, you will be responsible for managing financial records, handling accounting operations, and ensuring the accurate and efficient financial management of the company to support our rapidly growing team.

Key Responsibilities
Financial Record Keeping: Maintain accurate, up-to-date daily transaction records and accounting ledgers.
Financial Reporting: Prepare regular financial statements, income/expense reports, and present them to management in a timely manner.
Account Reconciliation: Perform bank reconciliations and verify transaction details to maintain financial integrity.
Compliance & Tax Management: Ensure all financial practices, tax filings, and regulatory requirements are fully compliant with relevant laws.
Team Collaboration: Work independently and collaborate effectively across departments to align financial tasks with overall company goals.


Qualifications & Requirements

Education & Experience: Relevant academic qualifications in Accounting, Finance, or a related field; prior hands-on accounting experience is required/preferred.
Communication Skills: Excellent communication and interpersonal skills to collaborate smoothly with team members and external stakeholders.
Work Style: Ability to work independently with minimal supervision, as well as function effectively as part of a team.
Professional Standards: Strong commitment, high integrity, professionalism, and a proactive willingness to learn and adapt.

HOW TO SUBMIT
WhatsApp: Send your documents to 0750 160 290
Email: Submit your application to info@domakatz.com
126 Watazamaji
HUSSEIN MAHAMUDU

Payroll Officer at Perseus Mining Limited September 2026

21 Sep 2026 • 16:46
Picha Payroll Officer at Perseus Mining Limited September 2026
Perseus Mining (Tanzania) Limited (SMLC) is seeking a Payroll Officer.

The Payroll Officer is responsible for the accurate, timely and compliant processing of employee payroll for a large-scale gold mining operation in Tanzania. The role ensures payroll records, earnings, statutory deductions, overtime, leave, employee changes and other payroll inputs are accurately captured, verified and processed in accordance with company policies, Tanzanian statutory requirements and internal controls. The position also supports payroll reporting, audits, employee payroll queries, pension submissions and continuous improvement of payroll processes, ensuring employees are paid accurately and on time.

Key Responsibilities
Work with the Accounts Payable and Payroll Superintendent to:

Review and verify payroll source documents.
Prepare and print payroll reports of earnings, hours worked, taxes, insurance, leave.
Develop, manage and maintain comprehensive payroll records.
Maintain a detailed annual payroll calendar of key payroll related tasks and due dates for planning purposes.
Verify all payroll changes, updates, and overtime into the payroll software system, ensuring the accuracy of the information entered.
Effect change note as required.
Ensure that all changes to payroll system are authorized as required.
Ensure that all changes to payroll system are authorized as required.
Ensuring compliance with tax regulations and company policies.
Ensure that all statutory and applicable deductions are captured to payroll system
Ensure that employees are paid correctly and on time.
Resolve all payroll related complaints
Ensure all new employees are correctly and timely captured
Ensure updated payroll record are timely sent to pension funds

Internal control
Audit

Responding to the queries raised i.e., provide support documents, information requested etc
Risk Management

Ensure Risk Minimisation strategies are in place.
All company assets are accounted for
Assist with Insurance for company assets.
Recommended Education Level

Bachelor of Commerce/ Bachelor of Accounting and Finance
Qualified Accountant (CPA-T) by the National Board of Accountants and Auditors Tanzania (NBAA) or the Association of Chartered Certified Accountant (ACCA) will be an added advantage.
Experience

Three years of experience in payroll process.
Experience in handling complex payroll for not less than 300 employees (full time and casual).

Knowledge and Skill
Reasonably independent and able to resolve own difficulties
Excellent knowledge of Group and local reporting requirements and accounting practices.
Excellent knowledge internal control requirement.
Good knowledge of payroll software and computer based financial accounting systems.
Totally honest and trustworthy.
Meticulous attention to detail.
Take responsibility to adhere to company procedures.
Must enjoy routine and take pride in producing accurate payroll outputs to meet deadlines on a regular basis.
Positive and enthusiastic to improve financial accounting performance.
Able to respond to heavy demands and high work pressure.
Timeously.
Qualifications & Licences:

Bachelor of Commerce/ Bachelor of Accounting and Finance
Qualified Accountant (CPA-T) by the National Board of Accountants and Auditors Tanzania (NBAA) or the Association of Chartered Certified Accountants (ACCA) will be an added advantage
Additional Information:

Prepared to undertake external training to complement the operation.
Incumbent may be expected to work outside Normal Working Hours on occasions.
Incumbent will, from time to time be required to travel on company business.
Risk Associated with Job

Commercial risk – High
Reputational risk – High
Application Mode:

Applications will only be received by email to perseus@globeconnect24-7.com with the advertised job title Payroll Officer as the subject line of the email.
126 Watazamaji
HUSSEIN MAHAMUDU

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI :FEMA MINING

21 Sep 2026 • 08:29
Picha TANGAZO LA NAFASI YA KAZI :FEMA MINING
Job description
Position: Maintenance Planner
Company: Fema Mining and Drilling Limited
Department: Maintenance / Technical Services
Location: Geita, Tanzania
Reports To: Project Superintendent
Job Type: Full-time

Job summary
Fema Mining and Drilling Limited is seeking a highly organized and technically competent Maintenance Planner to join our team. The Maintenance Planner will be responsible for planning, scheduling, and coordinating all preventive, predictive, and corrective maintenance activities for mining equipment, drilling rigs, and support machinery to ensure maximum equipment availability, reliability, and operational efficiency while minimizing downtime and costs.

Key responsibilities
Develop and maintain detailed maintenance schedules (preventive, predictive, and corrective) for all heavy mining equipment, drill rigs, vehicles, and plant machinery.
Create work orders, job plans, and maintenance procedures in the CMMS (Computerized Maintenance Management System).
Coordinate with Maintenance Supervisors, Technicians, Operations teams, and external contractors to ensure timely execution of maintenance activities.
Prepare weekly, monthly, and annual maintenance plans and forecasts.
Analyze equipment history, failure data, and performance trends to optimize maintenance strategies.
Ensure all maintenance activities comply with safety standards, OEM recommendations, and company policies.
Manage spare parts inventory by identifying critical spares, minimum stock levels, and procurement needs.
Track maintenance KPIs such as MTBF, MTTR, equipment availability, and backlog.
Participate in shutdown planning and major overhauls for drilling and mining equipment.
Liaise with suppliers and service providers for technical support and spare parts sourcing.
Continuously improve maintenance planning processes and implement best practices.
Qualifications and experience
Diploma or Bachelor’s Degree in Mechanical Engineering, Industrial Engineering, or a related technical field.
Minimum of 5 years of relevant experience in maintenance planning, preferably in the mining, drilling, or heavy equipment industry.
Proven experience working with heavy mobile equipment (excavators, dump trucks, drill rigs, dozers, etc.).
Strong knowledge and hands-on experience with CMMS systems (e.g., SAP, Pronto, Fiix, or similar).
Certification in Maintenance Planning or Reliability Engineering (e.g., CMRP) will be an added advantage.
Skills and competencies
Excellent planning, organizing, and time management skills.
Strong analytical and problem-solving abilities.
Good understanding of mining equipment maintenance practices and reliability principles.
Proficiency in Microsoft Office (especially Excel) and CMMS software.
Ability to read and interpret technical drawings, manuals, and OEM specifications.
Strong communication and interpersonal skills.
Ability to work under pressure and meet tight deadlines.
Knowledge of safety regulations and standards (e.g., OSHA, ISO 45001).
High level of integrity and attention to detail.
What we offer
Competitive salary and benefits package.
Medical insurance and other staff welfare benefits.
Opportunities for professional development and career growth in a growing mining company.
Dynamic and challenging work environment in the mining sector.
How to apply
Interested candidates should send their detailed CV, cover letter, and copies of relevant certificates to:
hr@fema-mining.co.tz
with the subject line “Application for Maintenance Planner”.

Application Deadline: 09TH October, 2026
132 Watazamaji
joseph joseph

MAONESHO YA TISA YA KITAIFA YA TEKINOLOJIA YA MADINI-GEITA

18 Sep 2026 • 11:42
Video
Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita inawakaribisha wachimbaji wa madini, kampuni, taasisi na wauzaji wa bidhaa za madini wajasiliamali na wananchi wote kushiriki katika maonesho ya tisa ya kitaifa ya teknolojia ya madini, kuanzia tarehe 23 Septemba hadi tarehe 3 Oktoba, 2026 katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Manispaa ya Geita" kauli Mbiu Madini ni Utajili tuwajibike pamoja ya kufikia dira ya taifa 2050." Maonesho haya yatafunguliwa na Mh: Dkt. Hussein Ally Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na yatafungwa na Mh:Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maonesho haya yataambatana na utoaji wa huduma za afya bure kwa wananchi , kutoka kwa watalaamu wa hospitali ya Benjamin Mkapa, MOI na NHIF. Lakini pia wananchi watapata huduma ya msaada wa kisheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na pia kutakuwa na vivutio vya wanyama pori na michezo ya watoto ili kushiriki, tembelea tovuti yetu ya www.madinigeita.co.tz au wasiliana nasi moja kwa moja, kupitia simu namba 0 7 9 32 62 34

IMARA CO VENTURES LIMITED Tutashirki Maonesho haya Usipange kukosa tutakuwa na bidhaa mbali mbali kama vile chimbo app and web app ,n.k
376 Watazamaji
HUSSEIN MAHAMUDU

SERIKALI KUTUMIA BILIONI 140 KUTAFITI MADINI NCHINI

18 Sep 2026 • 11:42
Video
Naibu Waziri Wizara ya Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesema katika mwaka wa fedha 2026/2027, Serikali inatarajia kutumia bilioni 140 kufanya utafiti wa kubaini madini yaliyopo nchini ili kuepukana na uchimbaji wa kubahatisha.

Akizungumza Septemba 16, 2026 mkoani Mwanza wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wajiolojia Tanzania (TGS) Mwaka 2026, Dkt. Kiruswa amesema kupitia utafiti huo watabaini maeneo gani wapewe wawekezaji au wachimbaji wakubwa na wadogo wa madini.

"Makusanyo hayo ya asilimia 10 mfano kwa mwaka huu wa fedha tunategemea kufikia Bilioni 140 ambazo zitatumika kwa ajili ya utafiti na kupitia uamuzi huo taasisi ya Jiolojia na utafiti wa madini Tanzania itawezeshwa katika shughuli za utafiti na hatimaye kupata taarifa nyingi za Jiosayansi," amesema.

Kwa upande wake Rais wa Jumuiya hiyo ya wanajiolojia, Profesa Elisante Mshiu, ameeleza shauku ya Jumuiya hiyo kuwa ni kuundwa kwa chombo au bodi itakayosimamia sekta hiyo ya madini ili kuondoa "vishoka".

Nao baadhi ya washiriki katika mkutano wamepongeza hatua ya Serikali kutenga fedha hizo kwa ajili ya utafiti huku wakidai kuwa itaenda kuleta mabadiliko katika sekta hiyo ya madini.
167 Watazamaji
HUSSEIN MAHAMUDU

WAZIRI WA MADINI AZINDUA RASMI MAANDALIZI YA MKUTANO MKUBWA WA MADINI NOVEMBA 2026

18 Sep 2026 • 11:28
Picha WAZIRI WA MADINI AZINDUA RASMI MAANDALIZI YA MKUTANO MKUBWA WA MADINI NOVEMBA 2026
Ni Mkutano mkubwa wa Madini na Uwekezaji

Washiriki 2000 kutoka mataifa 50 Duniani kushiriki

Kauli Mbiu ya Mkutano inalenga kuongeza thamani madini kwa maendelezo ya Viwanda

Serikali na Sekta Binafsi kushirikiana kuandaa mkutano huo


Waziri Mavunde azindua rasmi maandalizi ya mkutano huo

DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia S. Hassan anatarajiwa kufungua rasmi Mkutano wa Saba wa Madini na Uwekezaji Tanzania (TMIC 2026) utakaofanyika Novemba 19 hadi 21, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema serikali imeamua kujenga uchumi wa viwanda unaotokana na madini kwa kuwekeza katika uchakataji na uyeyushaji wa madini badala ya kuendelea kuuza malighafi.

Amesema kaulimbiu ya mkutano huo, "Madini Yaliyoongezwa Thamani: Chachu ya Ukuaji wa Viwanda na Uchumi," inaakisi dira ya serikali ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uchakataji wa madini barani Afrika.

Kwa mujibu wa Mhe. Mavunde, amesema Tanzania tayari ina viwanda vinane vya kusafisha dhahabu, huku Mkoa wa Dodoma ukiwa na viwanda tisa vinavyojengwa na vinavyoendelea na uzalishaji pamoja na kiwanda kikubwa cha kuyeyusha madini ya nikeli na shaba.

"Zaidi ya Sh bilioni 600 zinawekezwa katika ujenzi wa kiwanda cha chuma kitakachotumia asilimia 100 ya malighafi za ndani, huku uwekezaji mwingine ukiendelea Kigamboni na Tanga kwa ajili ya uchakataji wa madini ya 'Heavy Mineral Sands' na mradi wa madini ya niobium wa Panda Hill, Mbeya," amesema Mhe. Mavunde

Amesema, katika kuongeza ushiriki wa Watanzania kwenye sekta hiyo, thamani ya manunuzi kupitia mpango wa 'Local Content' imefikia Sh trilioni 5.1, huku bidhaa 20 zikitakiwa kuzalishwa na wazawa kwa ajili ya kuhudumia migodi mikubwa.

Amesisitiza wafanyabiashara kuzingatia uaminifu na viwango vya kimataifa ili kunufaika zaidi na fursa hizo.

Amesema sekta ya madini imeendelea kuimarisha mchango wake katika uchumi kwa kuingiza Sh trilioni 1.374 katika Mfuko Mkuu wa Serikali, kiwango kilichovuka lengo la Sh trilioni 1.2 kwa mwaka huu wa fedha.

Mhe. Mavunde, amesema Serikali imeidhinisha asilimia 10 ya mapato yote ya sekta ya madini kuelekezwa kwenye utafiti wa kina wa jiofizikia ili kuongeza maeneo yanayofahamika kuwa na madini kutoka asilimia 16 ya sasa hadi asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

Aidha, amesema Serikali inaandaa mfuko maalumu wa mikopo kwa wachimbaji wadogo, ambao licha ya changamoto za mitaji na teknolojia, wanachangia takribani asilimia 40 ya mapato ya sekta ya madini.

Katika hatua nyingine, amesema Serikali inaanza operesheni ya kufuta kidijitali leseni zote za madini zisizotumika. Wamiliki watakaoshindwa kuwasilisha taarifa ndani ya muda uliowekwa watapewa notisi ya siku 30 kabla ya leseni hizo kujifuta moja kwa moja.

Nae, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, amesema Serikali imejipanga kuhakikisha utajiri wa madini unakuwa chachu ya kukuza viwanda vya ndani, kuongeza ajira na kuimarisha uchumi kupitia uongezaji thamani badala ya kuishia kwenye uchimbaji pekee.

Amesema TMIC 2026 utawakutanisha viongozi wa Serikali, taasisi za fedha, kampuni za madini, wataalamu wa teknolojia, watafiti na wadau wengine kutoka duniani kote kujadili fursa za uwekezaji na maendeleo ya sekta hiyo.

"Huu ni wakati wa kuingia katika awamu mpya ya uwekezaji, ubunifu na ukuaji wa sekta ya madini nchini," amesema.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Chemba ya Migodi Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, amesema mkutano huo unatarajiwa kuwakutanisha washiriki zaidi ya 2,000 na watoa mada zaidi ya 100 kutoka mataifa zaidi ya 50, huku zaidi ya mada 20 zikijadiliwa zikiwemo sera, kodi, uwekezaji, teknolojia, nishati safi, madini ya kimkakati, uongezaji thamani na masuala ya mazingira, jamii na utawala bora (ESG).

Mchwampaka amesema TMIC 2026 pia utaweka mkazo katika maendeleo ya wachimbaji wadogo pamoja na ushirikishwaji wa wanawake na watu wenye ulemavu katika mnyororo mzima wa uongezaji thamani wa madini. Mkutano huo unatarajiwa kufungwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi.
167 Watazamaji
HUSSEIN MAHAMUDU

UKAGUZI WA MIGODI WAIMARISHA USALAMA, UHIFADHI WA MAZINGIRA

12 Sep 2026 • 08:07
Picha UKAGUZI WA MIGODI WAIMARISHA USALAMA, UHIFADHI WA MAZINGIRA
Tume ya Madini yasisitiza uchimbaji unaozingatia sheria, afya na maendeleo endelevu

?Dodoma

Tume ya Madini imeendelea kuimarisha ukaguzi wa migodi nchini ili kuhakikisha shughuli zote za uchimbaji zinafanyika kwa kuzingatia sheria, usalama wa wafanyakazi, afya kazini na utunzaji wa mazingira, hatua inayolenga kujenga sekta ya madini yenye tija na endelevu.

Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, Mjiolojia na Mkaguzi wa Migodi kutoka Tume ya Madini, Paschal Juma, amesema Kurugenzi ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira chini ya Mkurugenzi wake, Mhandisi Hamisi Kamando, ina jukumu la kusimamia na kufuatilia shughuli zote za uchimbaji ili kuhakikisha zinazingatia Sheria ya Madini, kanuni, sera na miongozo mbalimbali ya sekta hiyo.

Amesema Kurugenzi hiyo hufanya ukaguzi wa usalama na afya mahali pa kazi, hufuatilia utekelezaji wa mipango ya usimamizi wa mazingira, urejeshaji wa maeneo yaliyochimbwa pamoja na mipango ya ufungaji migodi kwa kuzingatia viwango vinavyolinda mazingira na kuhakikisha rasilimali za madini zinatumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Aidha, amesema Kurugenzi hiyo hupitia na kuidhinisha mipango ya uchimbaji, taarifa za utendaji wa migodi na usanifu wa miundombinu ya migodi, huku ikisimamia matumizi salama ya baruti kwa mujibu wa Sheria ya Baruti, Sura ya 45, na kanuni zake.

Paschal amesema Tume ya Madini inatumia Maonesho ya Nanenane kama jukwaa la kutoa elimu kwa wananchi, wachimbaji na wadau wa sekta kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga, mbinu salama za uchimbaji, utunzaji wa mazingira pamoja na uhifadhi na matumizi salama ya baruti.

Amesisitiza kuwa elimu hiyo inalenga kuongeza uelewa wa wadau, kuimarisha uzingatiaji wa sheria na viwango vya usalama, kupunguza ajali migodini na kuendeleza sekta ya madini inayochangia ukuaji wa uchumi wa taifa kwa njia endelevu.
331 Watazamaji
Joseph Malaika(JOMA)

KISARAWE YAJA NA SULUHU MAHITAJI YA BARUTI, VILIPUZI NCHINI

12 Sep 2026 • 08:03
Picha KISARAWE YAJA NA SULUHU MAHITAJI YA BARUTI, VILIPUZI NCHINI
?Kiwanda Kikubwa Afrika Mashariki Kuanza Uzalishaji Septemba,2026

?Dkt. Kiruswa Aahidi Serikali Kushughulikia Changamoto za Wawekezaji

?DC Magoti: Kisarawe Tayari kwa Mapinduzi ya Viwanda

? Kisarawe

Wilaya ya Kisarawe inaendelea kujijenga kuwa kitovu cha uzalishaji wa baruti na vilipuzi nchini, kufuatia kuanzishwa kwa viwanda viwili vinavyolenga kuongeza uzalishaji wa bidhaa hizo ndani ya nchi na kupunguza utegemezi wa uagizaji kutoka nje.

Viwanda hivyo ni Ideal Detonators Tanzania Limited, kinachotarajiwa kuwa miongoni mwa viwanda vikubwa vya aina hiyo katika Ukanda wa Afrika Mashariki, na Solar Intracom Chemicals Limited. Ideal kina uwezo wa kuzalisha tani 84,000 za baruti na vipande 50,000 vya vilipuzi kwa mwaka, huku Solar kikiwa na uwezo wa kuzalisha tani 25,000 za baruti na vipande 15,000 vya vilipuzi kwa mwaka.

Akizungumza wakati wa ziara yake Wilayani Kisarawe iliyolenga kukagua shughuli za madini, kufahamu changamoto za wawekezaji na kufuatilia utekelezaji wa miradi, Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, alisema uwepo wa viwanda hivyo utasaidia kuongeza upatikanaji wa baruti na vilipuzi vinavyohitajika katika shughuli za migodi na matumizi mengine nchini.

Alisema mahitaji ya baruti nchini yanakadiriwa kufikia wastani wa tani 79,548.22 kwa mwaka, pamoja na vipande 29,663.17 vya vilipuzi, hivyo uwekezaji huo ni muhimu kwa kuwa utaongeza uzalishaji wa ndani.

Dkt. Kiruswa alisema uwekezaji huo unaonesha utekelezaji wa dhana ya uongezaji thamani madini, kwa kuwa Tanzania inalenga siyo tu kuchimba madini, bali pia kuzalisha bidhaa zinazohitajika katika shughuli za uchimbaji hapa nchini.

“Baruti ni miongoni mwa bidhaa muhimu katika shughuli za madini, kwani huwezesha wachimbaji kuyafikia madini. Uzalishaji wa bidhaa hizi hapa nchini utaongeza upatikanaji wake na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje,” alisema Dkt. Kiruswa.

Kuhusu changamoto ya soko la ndani iliyowasilishwa na Solar Intracom Chemicals, Dkt. Kiruswa alisema Wizara inalichukua suala hilo kwa uzito na italishughulikia kwa kushirikiana na wadau, ili kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zinapata soko na viwanda vinaendelea kuzalisha.

Alisema ikiwa Serikali imeweza kushughulikia changamoto zilizowahi kujitokeza katika sekta nyingine za uzalishaji ikiwemo chumvi, hivyo ina imani kuwa changamoto zinazokabili uzalishaji wa baruti na vilipuzi nazo zitapatiwa ufumbuzi.

Vilevile, kuhusu changamoto ya vifaa kukaa bandarini kwa muda mredu iliyowasilishwa na kampuni ya Ideal Detonators, Dkt. Kiruswa alisema Serikali italifanyia kazi suala hilo kwa kushirikiana na mamlaka husika.

Kwa upande wake, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Lameck Gabote, alisema Tanzania ina jumla ya viwanda vinane (8) vidogo na vya kati vinavyozalisha wastani wa tani 49,000 za baruti na vipande 950,000 vya vilipuzi kwa mwaka.

"Pamoja na uzalishaji huo, bado haukidhi mahitaji ya matumizi ya baruti katika migodi nchini kwa mwaka. Kwa Mkoa wa Pwani una jumla ya viwanda vinne (4) vya kuzalisha baruti, ambapo viwili (2) kati yake vipo Wilaya ya Kisarawe," alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Petro Maguti, alisema wilaya hiyo iko tayari kwa mapinduzi makubwa ya viwanda, akibainisha kuwa Ideal Detonators ni miongoni mwa viwanda vikubwa vya aina hiyo katika Ukanda wa Afrika Mashariki, kikiwa na uwekezaji wa zaidi ya Shilingi bilioni 15.

Alisema Kisarawe inatarajia kupokea viwanda vingine vinne vinavyolenga kuzalisha bidhaa mbalimbali, ikiwemo nondo, spika na viwanda vya kutotolesha kuku.

“Kisarawe ina madini ya viwandani na ujenzi, maeneo ya kujenga viwanda, umeme, maji na miundombinu wezeshi ya usafirishaji. Tuko tayari kupokea uwekezaji zaidi,” alisema Mhe. Maguti.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na viwanda hivyo, kila kimoja tayari kimetoa ajira kwa takribani Watanzania 250, hivyo kuongeza fursa za ajira na shughuli za kiuchumi Wilayani Kisarawe.

Kiwanda cha Solar Intracom Chemicals Limited kilizinduliwa na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, na kuanza uzalishaji Agosti 14, 2026, huku Kiwanda cha Ideal Detonators Tanzania Limited kikitarajiwa kuanza uzalishaji Septemba 2026.
331 Watazamaji
Joseph Malaika(JOMA)

TANZANIA NA UINGEREZA WAIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA MADINI

11 Sep 2026 • 12:47
Picha TANZANIA NA UINGEREZA WAIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA MADINI
Leo jijini Dodoma, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mh. Marianne Young, amekutana na Waziri wa Madini, Mh. Anthony Mavunde, kwa ajili ya kujadili maendeleo ya sekta ya madini na fursa za kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza.

Mazungumzo hayo yalilenga uwekezaji, uongezaji thamani wa madini, na namna ya kuhakikisha sekta ya madini inaendelea kuchangia katika ukuaji wa uchumi jumuishi na endelevu.

????? Tanzania na Uingereza zitaendelea kushirikiana katika maeneo yenye manufaa kwa pande zote mbili kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa wananchi wa mataifa yote mawili.
340 Watazamaji
Joseph Malaika(JOMA)

Hakuna matokeo yaliyopatikana.

Anza Sasa